Education
Personal Experience
JUNIA 6, SURUALI MOJA: SAFARI YANGU YA KUJIFUNZA UKWELI
Mwaka 2021 niliondoka Mwanza nikiwa na mtaji wa TSh 2,000,000. Wakati huo nilikuwa mjasiriamali wa biashara ya mitumba. Nilikuwa na mtazamo kwamba fedha ndiyo kitu kikubwa kinachohitajika ili mtu afanye biashara au aanze shughuli inayoweza kumbadilishia m
Not the end, just a new beginning.
Lakini safari yangu ya kilimo ilinifundisha somo ambalo mpaka leo sijalisahau.
Nilielekeza sehemu ya fedha yangu kwenye kilimo. Nilikodi shamba lenye ukubwa wa ekari 10 kwa TSh 500,000 na nikapanda mahindi aina ya DK 77.
Nilikuwa nimeingia kwenye kilimo nikiwa na matumaini makubwa. Niliona ekari 10 kama nafasi kubwa ya kupata mavuno mazuri na kurudisha fedha niliyowekeza.
Lakini kilimo kilinifundisha tofauti.
Msimu wa kwanza ulipofika wakati wa mavuno, nilivuna. Nilikuwa nimepanga kichwani namna mavuno yangenisaidia kusonga mbele. Lakini nilipoanza kuona uhalisia wa mapato yangu, niligundua kuwa kilimo hakihitaji pesa pekee.
Kinahitaji maarifa, maandalizi, mipango na uelewa wa kile unachokifanya.
Wakati huo nilikuwa nanunua junia kwa takribani TSh 24,000.
Kilichoniumiza zaidi ni kuona namna thamani ya mavuno yangu ilivyokuwa ndogo ukilinganisha na matarajio niliyokuwa nayo.
Nilifika mahali ambapo nilijifunza kwa njia ambayo si rahisi kusahau:
Junia 6 ziliweza kuninunulia suruali moja tu.
Ndiyo maana nikaipa safari hii jina:
“Junia 6, Suruali Moja.”
Haikuwa tu kuhusu suruali.
Ilikuwa kuhusu mimi kugundua kwamba unaweza kuwa na pesa, unaweza kukodi ekari nyingi, unaweza kununua mbegu nzuri, lakini bado ukakosa matokeo uliyotarajia kama hujaelewa vizuri kilimo unachokifanya.
Mwaka uliofuata niliendelea na kilimo, na safari hii niliona tofauti kubwa. Nilivuna junia 24.
Hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwamba kilimo si suala la kusema tu, “Nina pesa, nitapanda.”
Kilimo ni mfumo.
Unahitaji kujua ardhi yako, mbegu unayotumia, maandalizi ya shamba, muda sahihi wa kupanda, namna ya kutunza zao, gharama zako na mwisho kabisa soko la mazao yako.
Safari yangu ilinifundisha pia kutokudharau hasara.






Comments 0
eacher | 🌱 Farmer | ✊ Activist 📚 Educating minds | 🌾 Growing food 🌍 Advocating for positive change 🇹🇿 Tanzania
Author
View profile